MAARIFA YA UFUGAJI KWA VITENDO
BY DIOFARM TZ

Morogoro, Tanzania
Simu: 0755051870
Email: dionezio81@gmail.com
UTANGULIZI
Ndugu mfugaji,Karibu kwenye mkusanyiko wa maarifa ya ufugaji yaliyokusanywa kwa vitendo kupitia uzoefu, changamoto na mafanikio ya kila siku. Elimu hii imelenga kukuimarisha wewe mfugaji ili ufugaji wako uwe wa tija na faida. Ufugaji si tu kazi ya kawaida, bali ni taaluma na biashara yenye nguvu kubwa ya kiuchumi.Kwa sasa ufugaji umekuwa ni nguzo kuu ya mafanikio ya wengi mijini na vijijini pia. Na tunaposema ufugaji hatumaanishi kitendo cha kujenga banda na kuweka kuku hapana, ufugaji lazima ufuate taratibu zote mhimu na lengo kuu lazima liwe biashara na kukuza uchumi.Karibu tujifunze pamoja.
SURA YA 1: MISINGI YA UFUGAJI BORA
Tambua lengo la mradi wako (biashara, kujifunza, n.k.)Msimamizi wa mradi ni nani?Kuandaa mazingira bora ya banda”Usichanganye malengo, elewa unataka nini kabla hujaanza.”Wengi wetu huanza ufugaji kwa sababu ameona jirani anafuga au ameona hana kazi nyingine matokeo yake anaanza ufugaji bila kujua lengo lake kuu ni nini.Hakikisha unaainisha lengo lako kabla ya kuanza eidha unafuga kuku kwa ajiri ya nyama, mayai au vyote.
SURA YA 2: BIOSECURITY NA USALAMA WA BANDA
Maana ya biosecurity: Ulinzi wa maishaYaani tunapofanya au kuzuia magonjwa ya kuku kuingia bandani lengo kuu ni kuokoa maisha ya kuku na kumfanya awe na afya njema muda wote.
Mbinu tatu kuu za biosecurity.
Isolation: Ili kuepuka magonjwa na athari hakikisha unatenga kuku wakubwa na wadogo yaani kama unafuga kuku wa rika tofauti usichanganye katika banda moja.Kama mtoa huduma mwangalizi ni mmoja hakikisha unaanza na kuku wadogo kwenda wakubwa hii itaepusha kusafirisha magonjwa kutoka kwa wakubwa kwenda kwa wadogo.Kwa mabanda yanayo angaliana madirisha yapishane walau mita 8 ili kuepusha magonjwa kusafiri kutoka banda moja kwenda jingine kwa njia ya hewa.
Traffic Control: Kwa ajiri ya kuwasaidia wageni ili wafuate sharia na taratibu zako, hakikisha umeweka vibao vya alama vitakavyo waongoza kuchukua hatua Fulani kama vile SIMAMA, NENDA, KATA KUSHOTO, KATA KULIA, Nk.. pia weka alama kuwaonesha maeneo yanayo ruhusiwa nay ale yasiyo ruhusiwa kama vile USIINGIE HAPA BILA RUHUSA.
Sanitation: Tumia dawa au viua vimelea kama vile V-RID, ULTRAXIDE, TH4, NORO CLEARANCE Nk.. ili kusafisha banda kabla nabaada ya kuku kuwepo bandani.Fuata maelekezo ya daktari. Nawa maji na kanyaga maji yenye dawa kabla ya kuingia bandani.Kwa uufupi;Tumia alama, weka taratibu, epuka vimelea”Treatment is more costly than prevention”
SURA YA 3: CHAKULA BORA KWA KUKU
Chakula ni sehemu kubwa ya mafanikio ya ufugaji (70% ya gharama).Tofauti ya lishe kwa broilers, layers, chotara na kienyeji.walishe kuku wako kwa utaratibu maalumu na usijaze tu vyombo vya chakula bila utaratibu. Tumia mfumo wa “Technical feeding”, yaani tambua mahitaji ya chakula kwa kuku wako na ujue ni muda gani kuku wako wanakula kwa amani na chakula cha kutosha na muda gani hawali.Mfano: kipindi cha joto mara nyingi kuku hula chakula zaidi muda wa usiku na siyo mchana, hivyo ukisha tambua hilo mchana weka chakula kidogo na usiku weka chakula cha kutosha. Epuka overfeeding au underfeeding yaani tambua chakula sahihi ambacho huwatosha kuku wako kwa siku kulingana na umri wao.
SURA YA 4: MBEGU NA MAKUNDI YA KUKU
Layers: kwa ajili ya mayai, mfano Hyaline Brown.
Broilers: kwa nyama, hukua haraka.
Chotara: mchanganyiko wa kienyeji na kisasa.
Kienyeji: wanaweza kustahimili mazingira magumu.
SURA YA 5: MALEZI YA VIFARANGA
Katika uleaji wa vifaranga umakini mkubwa unahitajika katika maandalizi.Vitu vya mhiu vya kuandaa;Banda bora safi na salama.Vyombo vya maji na chakulaGlucose na vitamini.Chanzo cha joto kwa siku 5–15 kulingana na hali ya hewa.Zingatia chanjo zote mhimu siku ya 7, 14,21 nk… kulingana na aina ya kuku.
SURA YA 6: TATHMINI NA UFUATILIAJI
Ili kuweza kuwa bora na kuendeleza ubora huu hakikisha unafanya yafuatayo;Pima uzito wa kuku wako kila baada ya siku 3-7 Linganisha matokeo(uzito) na viwango(standards) husika za uzitoShirikiana na wataalamu kufanya tathiini juu ya maendeleo ya kuku wako.Endapo utagundua uzito wa kuku wako hauendani na viwango vinavyo takiwa, fuatilia ujue sababu husika ya matokeo hayo.
SURA YA 7: SOKO NA BIASHARA YA UFUGAJI
My dear friend, tambua kuku katika biashara ya ufugaji kuna ushindani wa soko na ushindani huo mshindi huamliwa na vitu vikuu viwili ambavyo ni UBORA NA JUHUDI BINAFSI.
Tambua kuwa;Soko haliji bureTafuta kwa bidiiFanya hesabu ya gharama na bei ya kuuzaEpuka kuuza kwa hasaraJitofautishe kwa bidhaa bora na huduma nzuri.Tafuta kujua wapo soko lipo na lifuateHakikisha una fuatilia kujua taswira ya soko la bidhaa yako kabla hujaanza kufuga.Tambua kuwa ubora ndio silaha yako kuu, hivyo hakikisha kuku wako ni bora sana siku zote.
SURA YA 8: CHANGAMOTO NA SULUHISHO
Katika ufugaji changamoto zipo nyingi, hivyo kabla ya kuanza kufuga lazima uzifahamu na utafute njia za kuepuka changamoto hizo.Changamoto nyingi katika ufugaji husababisha na vitu kama vile;Mazingira ya uzalishaji wa kifaranga shambaniMazingira ya bandani kwakoChangamoto za uendeshajiHali ya hewa na mazingiraBanda lakoUzembe binafsi wa mfugajiKukosa elimu stahiki juu ya ufugaji.Hivyo ni vema unapoona changamoto yoyote kwa kuku wako kama vile magonjwa, ukuaji hafifu nk.. ni vema kufuatilia kujua chanzo kikuu cha titizo hilo na kama sababu kuu ni wewe basi fanya namna yoyote na utatue, lakini kama shida ni nje ya wewe tafuta pia suluhisho kulingana na chanzo husika.Ni vema kushirikiana na mtaalamu kubaini changamoto hizi na chanzo chake na kupata suluhisho kwa pamoja.
SURA YA 9: HUDUMA ZA DIOFARM NA ONE-ONE FEEDS
Ushauri wa kitaalamu kwa hatua zote.Chakula bora kwa aina zote za kuku.Concentrate kwa bei nafuu.ONE-ONE Feeds inapatikana nchi nzima.
HITIMISHO
Ndugu mfugaji,Ufugaji wa kisasa siyo tu kuwa na kuku na banda, bali ni kuwa na maarifa, mbinu, na mipango thabiti ya kufanikisha mradi kwa faida. Kupitia kitabu hiki, umepata mwongozo wa hatua kwa hatua unaokusaidia kuanza, kuimarisha, na kufanikisha mradi wako wa ufugaji.Changamoto zipo, lakini ukiwa na maarifa sahihi, mshauri wa karibu, na bidhaa bora kama chakula cha ONE-ONE Animal Feeds, unaweza kupiga hatua kubwa katika sekta hii ya muhimu.
Usiogope kuanza au kuanza tena. Mafanikio yako yapo kwenye utekelezaji wa maarifa.Ikiwa utahitaji msaada zaidi, usisite kuwasiliana na DIOFARM TZ. Elimu, ushauri na moyo wa kutaka ufanikiwe ni silaha zetu za pamoja.
Kumbuka: Ufugaji bora ni utajiri wa kweli.
DIOFARM TZ
Livestock MentorSimu: 0755051870
Email: dionezio81@gmail.com
Morogoro, Tanzania