Share this post on:

Shamba liandaliwe si chini ya miezi miwili (2) kabla ya kupanda kwa kuzingatia kanuni bora za uzalishaji wa zao la parachichi.

Mpangilio

  • Mbinu ya mpangilio wa shamba la parachichi inapaswa kulenga kutoa idadi ya juu zaidi ya miti kwa hekta, nafasi ya kutosha kwa ajili ya ukuzaji mzuri wa miti na kuhakikisha urahisi katika kulihudumia shamba.
  • Safu za shamba la parachichi zinapaswa kufuata mwelekeo wa jua (Mashariki – Magharibi) ili kuhakikisha mmea unapata mwanga wa jua wa kutosha.

Mifumo ya Upandaji

Mifumo ya upandaji inayotumika kwenye mashamba ya parachichi inategemea mwonekano wa shamba. Mifumo hiyo ni pamoja na:

Muundo wa Mraba

Inajumuisha upandaji wa miche katika mistari ya moja kwa moja na sambamba, ili kuwa na umbali sawia kati ya mmea na mmea na mstari na mstari. Mfumo huu unapendekezwa kwa mashamba yenye mteremko kati ya asilimia 0 hadi 5.

Upandaji wa pembe sita

Mimea huwekwa kwa usawa, na kutengeneza pembetatu sawa. Mfumo huu unaruhusu mimea zaidi ya asilimia 15 kwa kila eneo ikilinganishwa na muundo wa mraba. Unapendekezwa kwa mashamba yenye mteremko kati ya asilimia 5 hadi 15.

Mistari ya kontua

Mfumo huu hutumiwa katika mashamba yenye miteremko mikali ili kupunguza mmomonyoko wa udongo. Inapaswa kutumika katika mashamba yenye mteremko wa asilimia 15 hadi 45. Mfumo huu unaweza kutumika pamoja na aina nyingine za mipangilio (miundo ya mraba, pembesita na mstatili) kwa kuzingatia mistari ya kontua.

Nafasi za Upandaji

Nafasi za upandaji hutegemea sifa za ukuaji, aina ya parachichi, aina ya udongo, hali ya rutuba, ikolojia na kanuni za kilimo bora. Miche ipandwe kwa nafasi zilizopendekezwa kitalaam, kama inavyoainishwa katika Jedwali Na 3.

Jedwali Na 3: Nafasi za Upandaji wa Parachichi

Na.Mche kwa mche (mita)Mstari kwa Mstari (mita)Idadi ya Mche kwa Ekari
144250
255160
36974
448125
57963
Angalizo: Upandaji wa msongamano mkubwa (4m x 4m, 5m x 5m) hutoa mavuno bora katika miaka ya kwanza, ikizingatiwa vipandikizi vidogo, upogoaji wa kina wa miti wa mara kwa mara, unyunyiziaji vichocheo (hormoni) vinavyozuia ukuaji. Upandaji wa njia ya msongomano unashauriwa kutumika kwa wakulima wakubwa.

Upatikanaji wa Miche Bora ya Parachichi

Miche bora ya parachichi ni suala muhimu linalopaswa kuzingatiwa wakati wa upandaji. Mkulima anapaswa kupanda miche bora kutoka kwa wazalishaji wa miche waliosajiliwa na Taasisi ya Uthibiti Ubora wa Mbegu Tanzania (TOSCI). Wazalishaji wa miche ya parachichi watazalisha miche hiyo kwa kuzingatia viwango vya ubora vilivyotolewa na TOSCI, kwa mujibu wa Sheria ya Mbegu na Sheria ya Afya ya Mimea.

Maandalizi ya Shimo la Kupanda

  • Ukubwa wa shimo la kupandia unaoshauriwa kitaalam ni Sentimita (Sm) 60 kwa 60 kwa 60, na Sm 75 kwa sm 75 au mita 1 kwa mita 1 kwa mita 1 kwenye eneo lenye tabaka gumu la udongo.

Usimamizi wa Shamba

Umwagiliaji

Parachichi ni zao linalohitaji maji; zingatia kupima hali ya unyevu katika udongo kabla ya kumwagilia. Mahitaji ya maji kwa zao la parachichi yanatofautiana kutokana na majira na umri wa mti. Ufanisi na matokeo ya umwagiliaji huathiriwa na muda; inashauriwa kufanya umwagiliaji wakati wa asubuhi au jioni ambapo ardhi inakuwa imepoa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Need Help?