Share this post on:

Hivi ndivyo matajiri wanavyofanya Biashara ya mazao na kuzidi kutajirika…

1: Wengi wa matajiri hawazalishi wenyewe — wanamiliki mnyororo wa thamani:

HAWAISHI Mashambani, Lakini Wanamiliki Mzunguko Mzima

• Wananunua mazao kwa bei ya chini msimu wa mavuno.
• Wanayahifadhi kwenye maghala ya kisasa.
• Wanauza mazao hayo miezi kadhaa baadae kwa bei ya juu.

Wananunua mazao kama korosho, pamba, na mahindi kutoka kwa wakulima. Wana maghala makubwa, hivyo hawawezi kuuza kwa hasara wakati bei iko chini.

2. Wanatumia AKILI kuliko NGUVU

✅ Wanatumia taarifa za soko:
• Wanajua bei ya mahindi Songea, Dar, Mwanza, Mbeya na Kenya.
• Wanajua lini kuna uhaba, na wananunua kabla soko halijapanda.

Mfano. Unakuta ananunua gunia 10,000 za mahindi kwa TSh 55,000 wakati wa mavuno. Anayahifadhi na kuuza baada ya miezi 6 kwa TSh 95,000 kwa gunia. Faida: Milioni 400+ bila kulima hata eka moja.



3: Wanatumia MAGHALA NA GHARAMA KAMA UWEKEZAJI

✅ Wao hujenga au kukodisha maghala:
• Mazao hayaozi, hayaibiwi, hayashuki bei kirahisi.
• Wengine wanaingia mikataba na kampuni nyingine kwa ajili ya storage na resale.

Unakuta wanahifadhi mpunga au mahindi kwenye maghala kwa miezi 4-8 na kuuza kwa double price.

4. Wanapiga Hesabu Kabla ya Mvua Kunyesha

✅ Wanapanga kabla ya msimu:
• Wananunua mazao wakati watu wanakimbilia kuuza kwa hasara.
• Wanalenga kuuza wakati watu wana njaa au uhaba.

Mfano: Mwaka 2023, bei ya vitunguu kutoka Mang’ola ilikuwa TSh 20,000 kwa gunia msimu wa mavuno. Matajiri walinunua tani kwa tani, wakaweka store, wakaingiza sokoni mwezi Februari kwa TSh 80,000–90,000 kwa gunia.

5: Wanatumia VIBALI NA MITANDAO YA SOKO LA NJE

✅ Export ni sehemu kubwa ya utajiri wao:
• Wanapeleka choroko, ufuta, mbaazi, korosho, maharage, n.k. kwenye masoko ya India, China, na UAE.
• Wanalenga EXW (Ex-warehouse) prices—bei kabla bidhaa haijatoka ghala.

6: Wanatumia MIKATABA, VIKUNDI NA NGUVU YA MTANDAO

✅ Hawafanyi biashara kama mtu mmoja:
• Wako kwenye vikundi vya wafanyabiashara wakubwa.
• Wanagawana maghala, magari ya kusafirisha, na connection za nje.

🔑 SIRI KUU: “Wanakula faida ya hofu na ujinga wa wengine”

JE UNATAMANI KUJIFUNZA ZAIDI?

JUMAMOSI tarehe 2/8/2025 tutakua na semina ya Biashara ya nafaka ambayo tutafanya pale Golden Tulip Posta mpya.
.
Tutajifunza kiundani haya yote na zaidi kuanzia Mazao,machimbo, uendeshaji adi export

Hupaswi kukosa. Ada ya Ushiriki semina hii ni Tsh 50,000 tu kwenda lipa Voda 36180392 au Mpesa 0762260936 (Valentina Moi)kisha tuma message whatsapp kwa namba hiyohiyo usajiliwe.
.
Nafasi zimebaki chache na semina ni Jumamosi ijayo ya tarehe 2.
.

UNATAMANI KUFANYA HII BIASHARA?

Jambo gani unatamani kulijua kiundani zaidi…?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Need Help?