Share this post on:

Utangulizi

Parachichi, au Persea Americana, ni tunda lenye virutubisho muhimu sana kwa mwili wa binadamu. Tunda hili si tu linachangia afya, bali pia linasaidia kuongeza kipato kwa familia na taifa.

Aina za Parachichi

A: Parachichi za Asili Miti yake huwa mirefu lakini mavuno yake ni machache.

B: Aina za Kisasa/Chotara

Hass

Sifa kuu-lina vipere vipere sehemu ya juu ya ganda/ngozi yake, huchukua miezi 10-14 maeneo ya baridi kukomaa), uzito wa tunda ni gramu 150-300.

Fuerte

Ni aina ya chotara inayotokana na mchanganyiko wa aina za Guatemala na Mexico Sifa kuu lina ngozi nyembamba na laini. Hukomaa baada ya miezi 4-6 tangu mti wake ulipotoa maua na uzito wa tunda ni gramu 230-500.

X-Ikulu

Aina hii ni maarufu sana kwa mikoa ya nyanda za juu kusini (Njombe, Iringa, Mbeya na Ruvuma). Kiumbo tunda lake ni kubwa, majani yake ni mapana kama mti wa embe, rangi ya ganda ni kijani kabla na baada ya kuiva. Huchukua miezi sita kutoka maua hadi kukomaa na hukomaa wakati aina nyingine hazipo sokoni

Sehemu ya Kupanda

Pandisha maeneo yenye udongo usiotuamisha maji na wenye rutuba ili kuepuka magonjwa ya mizizi. Parachichi hustawi vizuri katika maeneo yenye mwinuko wa mita 1,500 – 2,100 kutoka usawa wa bahari na wastani wa mvua za mm 1,000.

Upandaji

Nafasi ya Upandaji

  • Mita 7 x 7 (miche 80-85)
  • Mita 8 x 8 (miche 60-65)
  • Mita 4 x 8 (miche 125-128)

Ukubwa wa Shimo Weka mashimo yenye ukubwa wa futi 3 x 3 x 3. Andaa mashimo haya miezi 2-3 kabla ya kupanda miche.

Umwagiliaji:

Ni muhimu kumwagilia miche ya parachichi ili kuongeza uzalishaji. Wakati wa kiangazi mwagilia angalao mara mbili kwa mwezi.

Umwagiliaji Umwagiliaji ni muhimu, hasa katika kipindi cha kiangazi. Mwagilia angalau mara mbili kwa mwezi.

Mbolea

Unaweza kutumia mbolea za asili (Samadi,Mboji) au za viwandani (DAP, Minjingu,NPK au TSP). Weka Samadi au Mboji,kilo 16 hadi 20 kwa shimo, mwezi moja kabla ya kupanda. Kwa mbolea za viwandani weka gramu 100 hadi 200 kwa shimo. Zingatia kuchanganya vizuri mbolea na udongo.

Kudhibiti Magugu

Weka shamba safi ili kuongeza uzalishaji. Dhibiti magugu kwa kutumia jembe au viua gugu vyenye viambata vya glyphosate.

Magonjwa na Wadudu

Parachichi hushambuliwa na magonjwa ya fangasi, ukungu,na wadudu. Dhibiti wadudu kwa kutumia viuatilifu kama lambdacyhalothrin, Indoxcarb na deltamethrin, mfano tumia sumu ya Ferrari gold FERRARI GOLD 522.5 EC na SHUJAA POWER 200 SC kutoka kampuni ya Agribase international bioscience.

Kudhibiti Ukungu:

Kwa matatizo ya ukungu, tumia viuatilifu vyenye viambata vyenye mancozeb, copper na metalax mfano ni JAZZ na RED COPPER (Nordox 75wg. wp na Nordox Express.

Uvunaji

Vuna parachichi zilizobebeshwa baada ya miaka miwili na nusu hadi mitatu. Epuka kuvuna wakati wa mvua na hakikisha kikonyo kinabaki kwenye tunda. Mti bora wenye miaka 4-5 unaweza kuzaa matunda 300-400 kwa mwaka, wakati mti wenye miaka 7 na kuendelea huzaa matunda 800-1,000 kwa mwaka. Aina ya Hass inauzwa kati ya Tsh 1000-1500 kwa kilo.

Kwa maelezo zaidi, wasiliana na: Meneja, Taasisi ya Utafiti wa Kilimo, TARI Kifyulilo, S.L.P 93 Mufindi. Simu: 0765176040 / 0769492549 Barua pepe: cmkifyulilo@tari.go.tz Tovuti: www.tari.go.tz

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Need Help?