Share this post on:

Uchaguzi wa eneo la kuanzisha shamba la parachichi ni uamuzi muhimu kwa ajili ya uzalishaji. Eneo lilipo shamba huathiri uzalishaji, ubora na masoko ya zao, uendelezaji wa shamba, udhibiti wa visumbufu vya mazao na ufikishaji wa mazao sokoni. Masuala muhimu ya kuzingatia katika uchaguzi wa eneo la shamba parachichi ni yafuatayo:

Aina ya Udongo

Parachichi hustawi vizuri kwenye udongo wenye uchachu (pH) kati ya 6 hadi 6.5 na unaopitisha maji kwa urahisi. Udongo haupaswi kuwa na tabaka gumu kwani utazuia kupenya kwa mizizi na inaweza kuathiri ukuaji mzuri wa mmea. Ni muhimu kupima afya ya udongo ili kubaini kiwango cha maboresho yanayohitajika.

Hali ya Hewa

Mmea wa parachichi hustawi vizuri katika maeneo yenye jotoridi la Sentigredi 10 hadi 30 na unyevu wa asilimia 75 hadi 80. Unyevu mwingi unaweza kusababisha ukungu kwenye shina, matawi na majani na kuathiri ukuaji wa maua na matunda. Kiasi cha mvua kinachohitajika ni milimita 1,000 hadi 2,000 kwa mwaka.

Mwinuko

Parachichi hustawi kutoka usawa wa bahari hadi mita 2,500; hata hivyo, zao hili hustawi vizuri zaidi kwenye mwinuko wa kuanzia mita 800 hadi 2,500 kutoka usawa wa bahari.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Need Help?